1 Nyakati

Sura: 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29

1 Nyakati 1


1 Adamu, na Sethi, na Enoshi;
2 na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi;
3 na Henoko, na Methusela, na Lameki;
4 na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.
5 Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
6 Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
7 Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.
8 Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
9 Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani.
10 Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
11 Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
12 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori.
13 Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi;
14 na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi;
15 na Mhivi, na Mwarki, na Msini;
16 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17 Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
18 Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi.
19 Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani.
20 Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera;
21 na Hadoramu, na Uzali, na Dikla;
22 na Obali, na Abimaeli, na Sheba;
23 na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24 Shemu, na Arfaksadi, na Sala;
25 na Eberi, na Pelegi, na Reu;
26 na Serugi, na Nahori, na Tera;
27 na Abramu, naye ndiye Ibrahimu.
28 Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli.
29 Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu;
30 na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema;
31 na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32 Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.
33 Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.
34 Na Ibrahimu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.
35 Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora.
36 Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki.
37 Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza.
38 Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani.
39 Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani.
40 Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana.
41 Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.
42 Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.
43 Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.
44 Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake.
45 Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake.
46 Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi.
47 Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake.
48 Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake.
49 Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake.
50 Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akamiliki badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.
51 Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi;
52 na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni;
53 na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari;
54 na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

1 Nyakati 2


1 Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;
2 na Dani, na Yusufu, na Benyamini, na Naftali, na Gadi, na Asheri.
3 Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; naye akamwua.
4 Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano.
5 Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli.
6 Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.
7 Na wana wa Karmi; Akani, yule mwenye kutaabisha Israeli, aliyekosa katika kitu kilichowekwa wakfu.
8 Na wana wa Ethani; Azaria.
9 Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.
10 Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;
11 na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi;
12 na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese;
13 na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;
14 na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;
15 na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;
16 na maumbu yao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.
17 Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli.
18 Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azubu, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni.
19 Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrathi, aliyemzalia Huri.
20 Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.
21 Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa mwenye miaka sitini; naye akamzalia Segubu.
22 Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
23 Na Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi, pamoja na Kenathi na miji yake, jumla yote miji sitini. Hao wote ni wana wa Makiri, babaye Gileadi.
24 Tena, baada ya kufa kwake Hesroni huko Kalebu-Efrata, ndipo Abia, mkewe Hesroni, alipomzalia Ashuri, babaye Teboa.
25 Na wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa Ramu, mzaliwa wa kwanza, na Buna, na Oreni, na Ozemu; kwa Ahiya.
26 Naye Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake Atara; yeye alikuwa mamaye Onamu.
27 Na wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, na Yamini, na Ekeri.
28 Na wana wa Onamu walikuwa Shamai, na Yada; na wana wa Shamai; Nadabu, na Abishuri.
29 Na mkewe Abishuri aliitwa jina lake Abihaili; naye akamzalia Abani, na Molidi.
30 Na wana wa Nadabu; Seledi, na Apaimu; walakini Seledi alikufa hana watoto.
31 Na wana wa Apaimu; Ishi. Na wana wa Ishi; Sheshani. Na wana wa Sheshani; Alai.
32 Na wana wa Yada, nduguye Shamai; Yetheri, na Yonathani; naye Yetheri akafa hana watoto.
33 Na wana wa Yonathani; Pelethi, na Zaza. Hao ndio wana wa Yerameeli.
34 Basi huyo Sheshani alikuwa hana wana wa kiume, ila binti. Naye Sheshani alikuwa na mtumwa, Mmisri, jina lake akiitwa Yarha.
35 Basi akamwoza binti yake aolewe na Yarha, mtumwa wake; naye akamzalia Atai.
36 Na Atai akamzaa Nathani; na Nathani akamzaa Zabadi;
37 na Zabadi akamzaa Eflali; na Eflali akamzaa Obedi;
38 na Obedi akamzaa Yehu; na Yehu akamzaa Azaria;
39 na Azaria akamzaa Helesi; na Helesi akamzaa Eleasa
40 na Eleasa akamzaa Sismai; na Sismai akamzaa Shalumu;
41 na Shalumu akamzaa Yekamia; na Yekamia akamzaa Elishama.
42 Na wana wa Kalebu, nduguye Yerameeli, walikuwa Mesha, mzaliwa wake wa kwanza, aliyekuwa babaye Zifu; na wana wa Maresha, babaye Hebroni.
43 Na wana wa Hebroni; Kora, na Tapua, na Rekemu, na Shema.
44 Naye Shema akamzaa Rahamu, babaye Yorkeamu; na Rekemu akamzaa Shamai.
45 Na mwana wake Shamai alikuwa Maoni; na Maoni alikuwa babaye Bethsuri.
46 Naye Efa, suria yake Kalebu, alimzaa Harani, na Mosa, na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi.
47 Na wana wa Yadai; Regemu, na Yothamu, na Geshani, na Peleti, na Efa, na Shaafu.
48 Naye Maaka, suria yake Kalebu, akamzalia Sheberi, na Tirhana.
49 Tena akamzaa Shaafu, babaye Madmana; na Sheva babaye Makbena; na babaye Gibea; naye binti Kalebu alikuwa Aksa.
50 Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;
51 Salma, babaye Bethlehemu; na Harefu, babaye Beth-gaderi.
52 Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi.
53 Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli.
54 Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori.
55 Na jamaa za waandishi waliokaa Yabesi; Watirathi, na Washimeathi, na Wasukathi. Hao ndio Wakeni, waliotoka kwake Hamathi, babaye mbari ya Rekabu.

1 Nyakati 3


1 Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli;
2wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi;
3wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe.
4Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akamiliki miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akamiliki miaka thelathini na mitatu.
5Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;
6na Ibhari, na Elishua, na Elipeleti;
7na Noga, na Nefegi, na Yafia;
8na Elishama, na Eliada, na Elifeleti, watu kenda.
9Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wana wa masuria; na Tamari alikuwa umbu lao.
10Na mwanawe Sulemani alikuwa Rehoboamu; na mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati;
11na mwanawe huyo ni Yehoramu; na mwanawe huyo ni Ahazia; na mwanawe huyo ni Yoashi;
12na mwanawe huyo ni Amazia; na mwanawe huyo ni Uzia; na mwanawe huyo ni Yothamu;
13na mwanawe huyo ni Ahazi; na mwanawe huyo ni Hezekia; na mwanawe huyo ni Manase;
14na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia.
15Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu.
16Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia.
17Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli,
18na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia.
19Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao;
20na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano.
21Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
22Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita.
23Na wana wa Nearia; Elioenai, na Hezekia, na Azrikamu, watu watatu.
24Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.

1 Nyakati 4


1 Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali.
2 Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi.
3 Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na umbu lao aliitwa jina lake Haselelponi;
4 na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, babaye Bethlehemu.
5 Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
6 Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara.
7 Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani.
8 Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu.
9 Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.
10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
11 Naye Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, aliyekuwa babaye Eshtoni.
12 Na Eshtoni akamzaa Beth-Rafa, na Pasea, na Tehina, babaye Ir-nahashi. Hao ni watu wa Reka.
13 Na wana wa Kenazi; Othnieli, na Seraya; na wana wa Othnieli; Hathathi.
14 Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye bonde la Wakarashi; kwani hao walikuwa mafundi.
15 Na wana wa Kalebu, mwana wa Yefune; Iru, na Ela, na Naamu; na wana wa Ela; na Kenazi.
16 Na wana wa Yehaleleli; Zifu, na Zifa, na Tiria, na Asareli.
17 Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa.
18 Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.
19 Na wana wa mkewe Hodia, umbu lake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka.
20 Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi.
21 Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa mbari ya wafuma nguo za kitani safi, wa mbari ya Ashbea;
22 na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. Na taarifa hizi ni za zamani sana.
23 Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.
24 Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli;
25 na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma.
26 Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei.
27 Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda.
28 Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali;
29 na huko Bilha, na Esemu, na Toladi;
30 na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi;
31 na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hata wakati wa kumiliki Daudi.
32 Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano,
33 na vijiji vyao vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo.
34 Naye Meshobabu, na Yamleki, na Yosha, mwana wa Amazia;
35 na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli;
36 na Elioenai, na Yaakoba, na Yeshohava, na Asaya, na Adieli, na Yesimieli, na Benaya;
37 na Ziza, mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya;
38 hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na mbari za baba zao zikaongezeka sana.
39 Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo zao malisho.
40 Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa na nafasi, tena imetulia, na kuwa na amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.
41 Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuzipiga hema zao, pamoja na hao Wameuni walioonekana huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo zao.
42 Na baadhi yao, maana ya hao wana wa Simeoni, watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi.
43 Nao wakawapiga mabaki ya Waamaleki waliookoka, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.

1 Nyakati 5


1 Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza.
2Kwani Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; bali haki ile ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu);
3wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.
4Wana wa Yoeli; mwanawe huyo ni Shemaya, na mwanawe huyo ni Gogu, na mwanawe huyo ni Shimei;
5na mwanawe huyo ni Mika, na mwanawe huyo ni Reaya, na mwanawe huyo ni Baali;
6na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni.
7Na nduguze kwa jamaa zao, hapo ilipohesabiwa nasaba ya vizazi vyao; mkuu wao, Yeieli, na Zekaria,
8na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hata kufika Nebo na Baal-meoni;
9na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng'ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.
10Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi.
11Na wana wa Gadi walikuwa wakikaa kwa kuwaelekea, katika nchi ya Bashani mpaka Saleka;
12Yoeli, alikuwa mkuu wao, na wa pili Shafamu, na Yanai, na Shafati, katika Bashani;
13na ndugu zao wa mbari za baba zao; Mikaeli, na Meshulamu, na Sheba, na Yorai, na Yakani, na Zia, na Eberi, watu saba.
14Hao ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yehishai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi;
15Ahi, mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa mkuu wa mbari za baba zao.
16Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake.
17Hao wote walihesabiwa kwa nasaba, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mfalme wa Israeli.
18Wana wa Reubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Manase, watu mashujaa, wawezao kuchukua ngao na upanga, na kupiga upinde, wenye ustadi katika kupigana vita, walikuwa watu arobaini na nne elfu mia saba na sitini, walioweza kwenda vitani.
19Nao wakapigana vita na Wahajiri; na Yeturi, na Nafishi, na Nodabu.
20Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.
21Wakateka nyara ng'ombe zao, na ngamia zao hamsini elfu, na kondoo zao mia mbili na hamsini elfu, na punda zao elfu mbili; na watu mia elfu.
22Kwani wengi walianguka waliouawa, kwa sababu vita vile vilikuwa vya Mungu. Nao wakakaa badala yao hata wakati wa ule uhamisho.
23Na wana wa nusu-kabila ya Manase walikaa katika nchi; nao wakaongezeka kutoka Bashani mpaka Baal-hermoni, na Seniri, na mlima Hermoni.
24Na hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao; Eferi, na Ishi, na Elieli, na Azrieli, na Yeremia, na Hodavia, na Yadieli; watu hodari wa vita, watu mashuhuri, wakuu wa mbari za baba zao.
25Nao wakamwasi Mungu wa baba zao, wakaenda kufanya uasherati na miungu ya watu wa nchi, ambao Mungu alikuwa amewaangamiza mbele yao.
26Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru na roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo.

1 Nyakati 6


1 Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
2 Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.
3 Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.
4 Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua;
5 na Abishua akamzaa Buki; na Buki akamzaa Uzi;
6 na Uzi akamzaa Zerahia; na Zerahia akamzaa Merayothi,
7 na Merayothi akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;
8 na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Ahimaasi;
9 na Ahimaasi akamzaa Azaria; na Azaria akamzaa Yohana;
10 na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu)
11 na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;
12 na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu;
13 na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria;
14 na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki;
15 na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo Bwana alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.
16 Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
17 Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei.
18 Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.
19 Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao.
20 Wa Gershoni; mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Yahathi, na mwanawe huyo ni Zima;
21 na mwanawe huyo ni Yoa, na mwanawe huyo ni Ido, na mwanawe huyo ni Zera, na mwanawe huyo ni Yeatherai.
22 Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;
23 na mwanawe huyo ni Elkana, na mwanawe huyo ni Ebiasafu, na mwanawe huyo ni Asiri;
24 na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli.
25 Na wana wa Elkana; Amasai, na Ahimothi.
26 Kwa habari za Elkana; wana wa Elkana; mwanawe huyo ni Sufu, na mwanawe huyo ni Tohu;
27 na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana.
28 Na wana wa Samweli; Yoeli, mzaliwa wa kwanza, na wa pili Abia.
29 Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza;
30 na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya.
31 Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi juu ya kazi ya kuimba katika nyumba ya Bwana, sanduku lile lilipokwisha pata mahali pa kustarehe.
32 Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya Bwana huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao.
33 Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;
34 mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;
35 mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;
36 mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli;
37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora;
38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.
39 Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;
40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya;
41 mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido;
42 mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei;
43 mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.
44 Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;
45 mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia;
46 mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri;
47 mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48 Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu.
49 Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu.
50 Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua;
51 na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia;
52 na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu;
53 na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi.
54 Basi haya ndiyo makao yao, sawasawa na marago yao mipakani mwao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza;
55 wakapewa Hebroni, katika nchi ya Yuda, na vijiji vyake vilivyouzunguka;
56 bali mashamba ya mji huo, na vijiji vyake, alipewa Kalebu, mwana wa Yefune.
57 Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake;
58 na Holoni pamoja na viunga vyake, na Debiri pamoja na viunga vyake;
59 na Ashani pamoja na viunga vyake, na Beth-shemeshi pamoja na viunga vyake;
60 tena katika kabila ya Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu.
61 Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hiyo, yaani, nusu-kabila, nusu ya Manase.
62 Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani.
63 Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Reubeni, na katika kabila ya Gadi, na katika kabila ya Zabuloni.
64 Na wana wa Israeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na viunga vyake.
65 Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila ya wana wa Yuda, na katika kabila ya wana wa Simeoni, na katika kabila ya wana wa Benyamini.
66 Na jamaa nyingine za wana wa Kohathi walikuwa na miji ya mipakani mwao katika kabila ya Efraimu.
67 Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake;
68 na Yokmeamu pamoja na viunga vyake, na Beth-horoni pamoja na viunga vyake;
69 na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake;
70 na katika nusu-kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi.
71 Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;
72 na katika kabila ya Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake;
73 na Remethi pamoja na viunga vyake, na En-gaminu pamoja na viunga vyake;
74 na katika kabila ya Asheri; Mishali pamoja na viunga vyake, na Abdoni pamoja na viunga vyake;
75 na Helkathi pamoja na viunga vyake, na Rehobu pamoja na viunga vyake;
76 na katika kabila ya Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake.
77 Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila ya Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake;
78 na ng'ambo ya mto wa Yordani huko Yeriko, upande wa mashariki wa Yordani, katika kabila ya Reubeni; Bezeri katika nyika pamoja na viunga vyake, na Yahasa pamoja na viunga vyake,
79 na Kedemothi pamoja na viunga vyake, na Mefaathi pamoja na viunga vyake;
80 na katika kabila ya Gadi; Ramothi katika Gileadi pamoja na viunga vyake, na Mahanaimu pamoja na viunga vyake;
81 na Heshboni pamoja na viunga vyake, na Yazeri pamoja na viunga vyake.

1 Nyakati 7


1 Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne.
2 Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa mbari za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu ishirini na mbili elfu na mia sita.
3 Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu.
4 Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi.
5 Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu themanini na saba elfu.
6 Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu.
7 Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu ishirini na mbili elfu na thelathini na wanne.
8 Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri.
9 Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu ishirini elfu na mia mbili.
10 Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari.
11 Hao wote ndio wana wa Yediaeli, sawasawa na wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, kumi na saba elfu na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.
12 Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri.
13 Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shilemu; wana wa Bilha.
14 Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;
15 naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.
16 Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.
17 Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18 Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.
19 Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.
20 Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi;
21 na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuzipokonya ng'ombe zao.
22 Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji.
23 Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu mna mabaya nyumbani mwake.
24 Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.
25 Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani;
26 na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama;
27 na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.
28 Na hizi ndizo hozi zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;
29 na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli.
30 Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera.
31 Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.
32 Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na umbu lao, Shua.
33 Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti.
34 Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu.
35 Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali.
36 Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra;
37 na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera.
38 Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara.
39 Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia.
40 Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa mbari za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, wakuu wa mashehe. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu ishirini na sita elfu.

1 Nyakati 8


1 Naye Benyamini akamzaa Bela, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Ashbeli, na wa tatu Ahiramu;
2 na wa nne Noha, na wa tano Rafa.
3 Na Bela alikuwa na wana; Adari, na Gera, na Abihudi;
4 na Abishua, na Naamani, na Ahoa;
5 na Gera, na Shufamu, na Huramu.
6 Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi;
7 na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi.
8 Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara.
9 Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu;
10 na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao.
11 Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali.
12 Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake;
13 na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi.
14 Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi;
15 na Zebadia, na Aradi, na Ederi;
16 na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria.
17 Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi;
18 na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali.
19 Na Yakimu, na Zikri, na Zabdi;
20 na Elienai, na Silethai, na Elieli;
21 na Adaya, na Beraya, na Shimrathi; walikuwa wana wa Shema.
22 Na Ishpani, na Eberi, na Elieli;
23 na Abdoni, na Zikri, na Hanani;
24 na Hanania, na Elamu, na Anthothiya;
25 na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki.
26 Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia;
27 na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu.
28 Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu.
29 Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka;
30 na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni, na Suri, na Kishi, na Baali, na Nadabu;
31 na Gedori, na Ahio, na Zekaria
32 Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.
33 Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.
34 Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.
35 Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi.
36 Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;
37 na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli;
38 naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli.
39 Na wana wa Esheki nduguye ni hawa; mzaliwa wake wa kwanza, Ulamu, na wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti.
40 Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini.

1 Nyakati 9


1 Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.
2 Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika hozi zao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.
3 Na huko Yerusalemu walikuwa wakikaa baadhi ya wana wa Yuda, na wana wa Benyamini, na wana wa Efraimu na Manase;
4 Uthai, mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imli, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
5 Na wa Washiloni; Asaya, mzaliwa wa kwanza, na wanawe.
6 Na wa wana wa Zera; Yeueli, na ndugu zao; watu mia sita na tisini.
7 Na wa wana wa Benyamini; Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;
8 na Ibneya, mwana wa Yerohamu; na Ela, mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu, mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya;
9 na ndugu zao, sawasawa na vizazi vyao; watu mia kenda na hamsini na sita. Watu hao wote ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, kwa kadiri ya mbari za baba zao.
10 Na katika makuhani; Yedaya, na Yehoyaribu, na Yakini;
11 na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;
12 na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; na Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yazera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri;
13 wakuu wa mbari za baba zao; pamoja na ndugu zao; watu elfu na mia saba na sitini; watu wenye ustadi waliofaa sana kwa kazi ya huduma ya nyumba ya Mungu.
14 Na katika Walawi; Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari;
15 na Bakbakari, na Hereshi, na Galali, na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu;
16 na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.
17 Na katika mabawabu; Shalumu, na Akubu, na Talmoni, na Ahimani, na ndugu zao; naye Shalumu alikuwa mkuu wao;
18 ambao tangu hapo walikuwa wakingojea penye lango la mfalme upande wa mashariki; hao ndio waliokuwa wangojezi wa rago la wana wa Lawi.
19 Naye Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; pamoja na nduguze wa mbari ya babaye, Wakora; walikuwa wakiisimamia kazi hiyo ya huduma, wenye ungojezi wa malango ya maskani; na baba zao walikuwa wamesimamia matuo ya Bwana, wakiyalinda maingilio;
20 naye Finehasi, mwana wa Eleazari, alikuwa mkuu wao hapo zamani, naye Bwana alikuwa pamoja naye.
21 Zekaria, mwana wa Meshelemia, alikuwa bawabu mlangoni pa ile hema ya kukutania.
22 Hao wote waliochaguliwa kuwa wangojezi wa malango walikuwa watu mia mbili na kumi na wawili. Nao wakahesabiwa kwa nasaba katika vijiji vyao, ambao Daudi na Samweli, huyo mwonaji, walikuwa wamewaweka katika kazi yao waliyoamaniwa.
23 Basi watu hao na wana wao walikuwa na usimamizi wa malango ya nyumba ya Bwana, yaani, nyumba ya maskani, kwa zamu.
24 Hao wangojezi walikuwapo pande zote nne, kuelekea mashariki, na magharibi, na kaskazini, na kusini.
25 Na ndugu zao, katika vijiji vyao, wakaamaniwa kuingia kila siku ya saba, zamu kwa zamu, ili kuwa pamoja nao;
26 kwa maana wale wangojezi wanne, waliokuwa wakuu, nao ni Walawi, walikuwa na kazi ya kuamaniwa, tena walikuwa juu ya vyumba na juu ya hazina katika nyumba ya Mungu.
27 Nao wakalala kandokando nyumbani mwa Mungu, kwa kuwa ulinzi wake ulikuwa juu yao, nayo ilikuwa kazi yao kuyafungua malango asubuhi baada ya asubuhi.
28 Na baadhi yao walikuwa na ulinzi wa vyombo vya huduma; kwani huingizwa kwa hesabu, na kutolewa kwa hesabu vile vile.
29 Na baadhi yao waliamaniwa kuviangalia vyombo vya nyumbani, na vyombo vyote vya Patakatifu; na kuwa juu ya unga safi, na divai, na mafuta, na ubani, na manukato.
30 Na baadhi ya wana wa makuhani waliweka tayari machanganyiko ya manukato.
31 Naye Matithia, Mlawi mmojawapo, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, Mkora, aliamaniwa kazi ya kuviangalia vitu vile vilivyookwa kaangoni.
32 Na baadhi ya ndugu zao, wa wana wa Wakohathi, walikuwa juu ya mikate ile ya Wonyesho, ili kuiandaa kila sabato.
33 Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku.
34 Hao walikuwa wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, katika vizazi vyao vyote, watu wakuu; nao walikuwa wakikaa huko Yerusalemu.
35 Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, na jina la mkewe aliitwa Maaka;
36 na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni; na Suri, na Kishi, na Baali, na Meri, na Nadabu;
37 na Gedori, na Ahio, na Zekaria, na Miklothi.
38 Na Miklothi akamzaa Shimea. Hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.
39 Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.
40 Na mwana wa Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.
41 Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea.
42 Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;
43 na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli;
44 naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli

1 Nyakati 10


1 Basi Wafilisti wakapigana juu ya Israeli; nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima Gilboa.
2 Nao Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe; Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli.
3 Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde.
4 Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao, wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.
5 Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa.
6 Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu; na nyumba yake yote wakafa pamoja.
7 Kisha watu wote wa Israeli, waliokuwa huko bondeni, walipoona ya kuwa wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.
8 Hata ikawa siku ya pili yake Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara hao waliouawa, walimwona Sauli na wanawe wameanguka juu ya mlima Gilboa.
9 Wakamvua mavazi, wakamtwalia kichwa, na silaha zake, kisha wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari kwa sanamu zao, na kwa watu.
10 Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa miungu yao, wakakikaza kichwa chake nyumbani mwa Dagoni.
11 Na watu wote wa Yabesh-gileadi waliposikia hayo yote Wafilisti waliyomtenda Sauli,
12 wakainuka mashujaa wote, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi, wakaizika mifupa yao chini ya mwaloni huko Yabeshi, nao wakafunga muda wa siku saba.
13 Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,
14 asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.

1 Nyakati 11


1 Ndipo Israeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.
2 Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye Bwana, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli.
3 Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za Bwana; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la Bwana kwa mkono wa Samweli.
4 Kisha Daudi na Israeli wote wakaenda Yerusalemu, (ndio Yebusi;) nao Wayebusi, wenyeji wa nchi, walikuwamo.
5 Na hao wenyeji wa Yebusi wakamwambia Daudi, Hutaingia humu. Walakini Daudi akaitwaa ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi.
6 Naye Daudi akasema, Mtu ye yote atakayekuwa wa kwanza wa kuwapiga Wayebusi, yeye atakuwa mkuu na jemadari. Naye wa kwanza aliyepanda ni Yoabu mwana wa Seruya, naye akawa mkuu.
7 Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo huuita mji wa Daudi.
8 Akaujenga huo mji pande zote, toka Milo na kuuzunguka; naye Yoabu akautengeneza mji uliosalia.
9 Naye Daudi akaendelea, akazidi kuwa mkuu; kwa maana Bwana wa majeshi alikuwa pamoja naye.
10 Basi hawa ndio wakuu wa mashujaa aliokuwa nao Daudi, waliojitia nguvu pamoja naye katika ufalme wake, pamoja na Israeli wote, ili kumfanya awe mfalme, sawasawa na neno la Bwana alilonena juu ya Israeli.
11 Na hii ndiyo hesabu ya hao mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu, Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua pamoja.
12 Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu.
13 Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pasdamimu; ndiko Wafilisti walikokusanyika vitani, palipokuwa na konde limejaa shayiri ;na hao watu wakakimbia mbele ya wafilisti.
14 Ndipo hao wakasimama katikati ya konde lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu.
15 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hata pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai.
16 Na Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na walinzi wa Wafilisti wakati ule walikuwa huko Bethlehemu.
17 Naye Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!
18 Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana;
19 akasema, Mungu wangu apishe mbali, nisifanye hivi; je! Ninywe damu ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Maana kwa hatari ya nafsi zao wameyaleta. Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
20 Tena Abishai, nduguye Yoabu, alikuwa mkuu wa wale watatu; kwa kuwa aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua; akawa na jina kati ya wale watatu.
21 Katika wale watatu yeye alikuwa mwenye heshima kuliko hao wawili, akawa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu.
22 Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu; pia akashuka ,akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theruji.
23 Huyo akamwua Mmisri, mtu mrefu sana, aliyekuwa wa dhiraa tano urefu wake; na yule Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi; lakini yeye akamshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.
24 Mambo hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu.
25 Tazama, alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu; naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.
26 Tena hawa ndio mashujaa wa majeshi ya askari; Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethlehemu;
27 Shama Mharodi, Helesi Mpeloni;
28 Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abiezeri Mwanathothi;
29 Sibekai Mhushathi, Salmoni Mwahohi;
30 Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathi;
31 Itai mwana wa Ribai wa Gibea wa wana wa Benyamini, Benaya Mpirathoni;
32 Hurai wa vijito vya Gaashi, Abieli Mwaibathi;
33 Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni;
34 wana wa Yasheni Mgiloni, Yonathani mwana wa Shama Mharari;
35 Ahiamu mwana wa Sharari Mharari, Elifeleti mwana wa Ahasbai; Heferi
36 Mmaakathi, Ahia Mpeloni;
37 Hezro Mkarmeli, Paarai mwana wa Ezbai Mwarki;
38 Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri;
39 Seleki Mwamoni, Naharai Mbeorothi, mchukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya;
40 Ira Mwithri, Garebu Mwithri;
41 Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai;
42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni, mkuu wa Wareubeni, na thelathini pamoja naye;
43 Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithni;
44 Uzia Mwashterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri;
45 Yediaeli mwana wa Shimri, na Yoha nduguye, Muzi;
46 Elieli Mmahawi, na Yeribai, na Yoshavia, wana wa Elnaamu, na Ithma Mmoabi;
47 Elieli, na Obedi, na Yaasieli Mmesobai.

1 Nyakati 12


1 Basi hawa ndio wale waliomjia Daudi huko Siklagi, alipokuwa akijificha kwa ajili ya Sauli, mwana wa Kishi; nao walikuwamo miongoni mwa wale mashujaa, waliomsaidia vitani.
2 Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini.
3 Mkubwa wao alikuwa Ahiezeri, kisha Yoashi, wana wa Shemaa Mgibeathi; na Yezieli, na Peleti, wana wa Azmawethi; na Beraka, na Yehu Mwanathothi;
4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;
5 Eluzai, na Yerimothi, na Bealia, na Shemaria, na Shefatia Mharufi;
6 Elkana, na Ishia, na Azaleli, na Yoezeri, na Yashobeamu, Wakora;
7 na Yoela, na Zebadia, wana wa Yerohamu, wa Gedori.
8 Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;
9 Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu;
10 Mishmana wa nne, Yeremia wa tano;
11 Atai wa sita, Elieli wa saba;
12 Yohana wa nane, Elzabadi wa kenda;
13 Yeremia wa kumi, Makbanai wa kumi na moja.
14 Hao wa wana wa Gadi walikuwa maakida wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu.
15 Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
16 Tena wakafika ngomeni kwa Daudi baadhi ya wana wa Benyamini na Yuda.
17 Naye Daudi akatoka ili kuwalaki, akajibu, akawaambia, Kama mmenijia kwa amani ili kunisaidia, basi moyo wangu utaambatana nanyi; lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu, kwa kuwa hamna udhalimu mikononi mwangu, Mungu wa baba zetu na alitazame neno hili, na kulikemea.
18 Ndipo roho ikamjilia Abishai, mkuu wa wale thelathini, naye akasema, Sisi tu watu wako, Ee Daudi; Na wa upande wako, Ee mwana wa Yese; Amani, naam, amani iwe kwako, Na amani iwe kwao wakusaidiao; Maana akusaidiye ndiye Mungu wako. Ndipo Daudi akawakaribisha, akawaweka wawe maakida wa kile kikosi.
19 Wa Manase pia wengine walimwangukia Daudi, alipokwenda pamoja na Wafilisti juu ya Sauli vitani, lakini hawakuwasaidia; kwani wale mabwana wa Wafilisti wakafanya shauri, wakamfukuza, wakisema, kwa hatari ya vichwa vyetu atamwangukia bwana wake Sauli.
20 Naye alipokuwa akienda Siklagi, wakamwangukia hawa wa Manase, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, maakida wa maelfu waliokuwa wa Manase.
21 Wakamsaidia Daudi juu ya kile kikosi kilichomshambulia; kwani walikuwa waume mashujaa wote, nao wakawa maakida jeshini.
22 Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
23 Na hizi ni hesabu za vichwa vya watu wenye silaha za vita, waliokuja Hebroni kwa Daudi, ili kumgeuzia ufalme wa Sauli, sawasawa na neno la Bwana.
24 Wana wa Yuda, waliochukua ngao na mkuki, walikuwa elfu sita na mia nane, wenye silaha za vita.
25 Wa wana wa Simeoni, waume mashujaa wa vita, elfu saba na mia moja.
26 Wa wana wa Lawi, elfu nne na mia sita.
27 Na Yehoyada alikuwa kichwa cha mbari ya Haruni, na pamoja naye walikuwa elfu tatu na mia saba;
28 tena Sadoki, kijana shujaa, na wa nyumba ya babaye, maakida ishirini na wawili.
29 Na wa wana wa Benyamini nduguze Sauli, elfu tatu; kwani hata sasa walio wengi wao walikuwa wameuhifadhi uaminifu wao kwa nyumba ya Sauli.
30 Na wa wana wa Efraimu, ishirini elfu na mia nane, waume mashujaa, watu wenye sifa katika mbari za baba zao.
31 Na wa nusu kabila ya Manase, kumi na nane elfu, waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme.
32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
33 Wa Zabuloni, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, wenye zana za vita za kila namna, hamsini elfu; askari wastadi wasiokuwa wenye moyo wa kusita-sita.
34 Na wa Naftali, maakida elfu, na pamoja nao watu wenye ngao na mkuki thelathini na saba elfu.
35 Na wa Wadani, watu hodari wa kupanga vita, ishirini na nane elfu na mia sita.
36 Na wa Asheri, watu wawezao kwenda pamoja na jeshi, hodari wa kupanga vita, arobaini elfu.
37 Tena, ng'ambo ya pili ya Yordani, wa Wareubeni, na wa Wagadi, na wa nusu kabila ya Manase, wenye zana za vita za kupigania za kila namna, mia na ishirini elfu.
38 Hao wote, watu wa vita, askari wastadi, wakaja Hebroni wenye moyo mkamilifu, ili kumtawaza Daudi awe mfalme juu ya Israeli wote; tena wote waliosalia wa Israeli nao walikuwa na moyo mmoja kwamba wamtawaze Daudi.
39 Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari.
40 Zaidi ya hayo, wale waliokuwa karibu nao, hata mpaka kwa Isakari, na Zabuloni, na Naftali, wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng'ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng'ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli.

1 Nyakati 13


1 Kisha Daudi akafanya shauri na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, naam, na kila kiongozi.
2 Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa Bwana, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;
3 nasi tujirudishie tena sanduku la Mungu wetu; maana hamkuuliza neno kwa hilo katika siku za Sauli.
4 Nao jamii nzima wakasema ya kwamba watafanya hivyo; kwa kuwa neno hilo lilikuwa jema machoni pa watu wote.
5 Basi Daudi akawakusanya Israeli wote, toka Shihori, kijito cha Misri, hata pa kuingilia Hamathi, ili kwamba walilete sanduku la Mungu kutoka Kiriath-yearimu.
6 Basi Daudi akapanda, yeye na Israeli wote, mpaka Baala, ndio Kiriath-yearimu, ulio wa Yuda, ili kulileta toka huko sanduku la Mungu, Bwana akaaye juu ya makerubi, lililoitwa kwa Jina lake.
7 Wakalipandisha sanduku la Mungu juu ya gari jipya kutoka nyumba ya Abinadabu; na Uza na Ahio wakaliendesha lile gari.
8 Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.
9 Hata walipofika penye uga wa Nakoni, Uza akaunyosha mkono wake alishike sanduku; kwa maana wale ng'ombe walikunguwaa.
10 Ndipo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Uza, naye akampiga, kwa sababu alilinyoshea sanduku mkono wake, hata akafa pale pale mbele za Mungu.
11 Naye Daudi akaona uchungu, kwa kuwa Bwana amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo.
12 Naye Daudi akamwogopa Mungu siku ile, akasema, Nitajileteaje sanduku la Mungu kwangu?
13 Basi Daudi hakujichukulia sanduku mjini mwa Daudi, ila akalihamisha kando na kulitia nyumbani kwa Obed-edomu Mgiti.
14 Sanduku la Mungu likakaa na jamaa ya Obed-edomu, nyumbani mwake, muda wa miezi mitatu; naye Bwana akaibariki nyumba ya Obed-edomu, na yote aliyokuwa nayo.

1 Nyakati 14


1 Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba.
2 Daudi akajua ya kwamba Bwana amemweka imara ili amiliki juu ya Israeli, kwa kuwa milki yake imeinuka kwa ajili ya watu wake Israeli.
3 Tena Daudi akazidi kuoa wake huko Yerusalemu; akazidi Daudi kuzaa wana na binti.
4 Na haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani;
5 na Ibhari, na Elishua, na Elpeleti;
6 na Noga, na Nefegi, na Yafia;
7 na Elishama, na Eliada, na Elifeleti.
8 Na waliposikia hao Wafilisti ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao.
9 Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kuteka nyara katika bonde la Warefai.
10 Daudi akamwuliza Mungu, kusema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye Bwana akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.
11 Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, Bwana amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.
12 Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto.
13 Lakini hao Wafilisti wakateka nyara tena mara ya pili bondeni.
14 Na Daudi akamwuliza Mungu tena; naye Mungu akamwambia, Hutapanda kuwafuata; uwageukie mbali, ukawajie huko kuielekea miforsadi.
15 Kisha itakuwa utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miforsadi, ndipo utakapokwenda nje vitani; kwa maana ndipo Mungu ametoka mbele yako, awapige jeshi la Wafilisti.
16 Daudi akafanya kama vile Mungu alivyomwamuru; wakawapiga jeshi la Wafilisti toka Geba mpaka Gezeri.
17 Sifa za Daudi zikafika nchi zote; naye Bwana akawaletea mataifa yote hofu yake.

1 Nyakati 15


1 Basi Daudi akajifanyia nyumba katika mji wa Daudi; akapaweka tayari mahali kwa ajili ya sanduku la Mungu, akalipigia hema.
2 Ndipo Daudi akasema, Haimpasi mtu awaye yote kulichukua sanduku la Mungu, isipokuwa Walawi peke yao; kwa kuwa hao ndio aliowachagua Bwana, ili walichukue sanduku la Mungu, na kumtumikia daima.
3 Basi Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu, ili kulipandisha sanduku la Bwana, mpaka mahali pake alipoliwekea tayari.
4 Daudi akawakutanisha wana wa Haruni, na Walawi;
5 wa wana wa Kohathi; Urieli mkuu wao, na nduguze mia na ishirini;
6 wa wana wa Merari; Asaya mkuu wao, na nduguze mia mbili na ishirini;
7 wa wana wa Gershoni; Yoeli mkuu wao, na nduguze mia na thelathini;
8 wa wana wa Elsafani; Shemaya mkuu wao, na nduguze mia mbili;
9 wa wana wa Hebroni; Elieli mkuu wao, na nduguze themanini;
10 wa wana wa Uzieli; Aminadabu mkuu wao, na nduguze mia na kumi na wawili.
11 Tena, Daudi akawaita Sadoki na Abiathari makuhani, na hao Walawi, Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli, na Aminadabu,
12 akawaambia, Ninyi ni vichwa vya mbari za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipoliwekea tayari.
13 Kwani kwa sababu ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, Bwana, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta sawasawa na sheria.
14 Basi makuhani na Walawi wakajitakasa, ili wapate kulipandisha sanduku la Bwana, Mungu wa Israeli.
15 Na wana wa Walawi wakalichukua sanduku la Mungu mabegani mwao kwa miti yake, kama vile Musa alivyoamuru, sawasawa na neno la Bwana.
16 Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha.
17 Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi;
18 na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu.
19 Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;
20 na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi;
21 na Matithiya, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, na Azazia, wenye vinubi vya sauti ya Sheminithi,
22 waongoze. Na Kenania, mkuu wa Walawi, alikuwa juu ya uchukuzi; yeye aliusimamia uchukuzi, kwa sababu alikuwa mstadi.
23 Na Berekia na Elkana walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku.
24 Na Shebania, na Yoshafati, na Nethaneli, na Amasai, na Zekaria, na Benaya, na Eliezeri, makuhani, wakapiga baragumu mbele ya sanduku la Mungu; na Obed-edomu na Yehia walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku.
25 Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na maakida wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la agano la Bwana kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;
26 hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la agano la Bwana, wakachinja ng'ombe saba, na kondoo waume saba.
27 Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
28 Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la Bwana kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi.
29 Hata ikawa, sanduku la agano la Bwana lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.

1 Nyakati 16


1 Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.
2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana.
3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.
4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli;
5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;
6 nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la agano la Mungu.
7 Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana, kwa mkono wa Asafu na nduguze.
8 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake.
9 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote.
10 Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana.
11 Mtakeni Bwana na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.
12 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
13 Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake, Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14 Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake.
15 Likumbukeni agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
16 Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka;
17 Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri, Na Israeli liwe agano la milele.
18 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa;
19 Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa; Naam, watu wachache na wageni ndani yake.
20 Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.
21 Hakumwacha mtu awaonee; Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao;
22 Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.
23 Mwimbieni Bwana, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
24 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.
25 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
26 Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.
27 Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake.
28 Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.
29 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;
30 Tetemekeni mbele zake, nchi yote.
31 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, Bwana ametamalaki;
32 Bahari na ivume na vyote viijazavyo; Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;
33 Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,
34 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
35 Nanyi mkaseme, Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe, Utukusanye kwa kututoa katika mataifa, Tulishukuru jina lako takatifu, Tuzifanyie shangwe sifa zako.
36 Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi Bwana.
37 Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la agano la Bwana, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake.
38 Naye Obed-edomu, pamoja na ndugu zao, sitini na wanane; Obed-edomu na mwana wa Yeduthuni, na Hosa, wawe mabawabu;
39 na Sadoki kuhani, na nduguze makuhani, mbele ya maskani ya Bwana katika mahali pa juu palipokuwa huko Gibeoni,
40 ili kumtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya Bwana, aliyowaamuru Israeli;
41 na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru Bwana, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;
42 na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni.
43 Kisha watu wote wakaenda zao kila mtu nyumbani kwake; naye Daudi akarudi ili awabariki watu wa nyumbani mwake.

1 Nyakati 17


1 Ikawa, Daudi alipokuwa akikaa nyumbani mwake, Daudi akamwambia nabii Nathani, Angalia, mimi ninakaa katika nyumba ya mwerezi, bali sanduku la agano la Bwana linakaa chini ya mapazia.
2 Naye Nathani akamwambia Daudi, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; kwa maana Mungu yu pamoja nawe.
3 Ikawa usiku uo huo, neno la Mungu likamjia Nathani, kusema,
4 Nenda, kamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, Wewe hutanijengea nyumba ya kukaa;
5 kwa maana sikukaa ndani ya nyumba tangu siku ile nilipowaleta Israeli huku hata leo; lakini hema kwa hema nimehamia, na maskani kwa maskani.
6 Katika mahali mwote nilimokwenda na Israeli wote, je! Nimesema neno lo lote na mtu ye yote wa waamuzi wa Israeli, niliowaagiza kuwalisha watu wangu, nikisema, Mbona hamkunijengea nyumba ya mwerezi?
7 Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli;
8 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
9 Tena nitawaagizia watu wangu Israeli mahali, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena kama hapo kwanza,
10 na tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi wawe juu ya watu wangu Israeli, nami nitawashinda adui zako wote. Pamoja na hayo nakuambia, ya kwamba Bwana atakujengea nyumba.
11 Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende na babazo, nitainua mzao wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitaufanya imara ufalme wake.
12 Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele.
13 Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; wala sitamwondolea fadhili zangu, kama nilivyomwondolea yeye aliyekuwa kabla yako;
14 ila nitamstarehesha katika nyumba yangu na katika ufalme wangu milele; na kiti chake cha enzi kitathibitishwa milele.
15 Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote, ndivyo Nathani alivyonena na Daudi.
16 Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za Bwana; akasema Mimi ni nani, Ee Bwana Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa?
17 Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Mungu; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumwa wako, kwa miaka mingi inayokuja, nawe umeniangalia sawasawa na hali ya mtu mwenye cheo, Ee Bwana Mungu.
18 Na Daudi akuambie nini tena zaidi kwa habari ya heshima aliyotendewa mtumwa wako? Kwa maana wewe umemjua mtumwa wako.
19 Ee Bwana, kwa ajili ya mtumwa wako, na kwa moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote.
20 Ee Bwana, hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu mwingine ila wewe, kwa kadiri tulivyosikia kwa masikio yetu.
21 Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake mwenyewe, ili wawe watu wake, na kujifanyia jina kwa njia ya mambo makuu, yenye kuogofya, kwa kufukuza mataifa mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri?
22 Kwa maana watu wako Israeli ndio uliowafanya kuwa watu wako wa milele; nawe, Bwana, umekuwa Mungu wao.
23 Basi sasa, Ee Bwana, neno lile ulilolinena katika habari za mtumwa wako, na katika habari za nyumba yake, na lifanywe imara milele, ukafanye kama ulivyosema.
24 Jina lako na liwe imara, likatukuzwe milele, kusema, Bwana wa majeshi ndiye Mungu wa Israeli, naam, Mungu juu ya Israeli; na hiyo nyumba ya Daudi mtumwa wako imefanywa imara mbele zako.
25 Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumwa wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumwa wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako.
26 Na sasa, Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu, nawe umemwahidia mtumwa wako jambo hili jema;
27 nawe sasa umekuwa radhi kuibarikia nyumba ya mtumwa wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, Bwana, umebarikia, nayo imebarikiwa milele.

1 Nyakati 18


1 Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda, akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa Wafilisti.
2 Akapiga Moabu; na hao Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi wakaleta zawadi.
3 Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mamlaka yake kwenye mto wa Frati.
4 Daudi akampokonya magari elfu, na wapanda farasi saba elfu, na askari waendao kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia akawaweka.
5 Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akapiga katika hao Washami watu ishirini na mbili elfu.
6 Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
7 Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumishi wa Hadadezeri akazileta Yerusalemu.
8 Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyofanyizia Sulemani ile bahari ya shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba.
9 Hata aliposikia Tou, mfalme wa Hamathi, ya kuwa Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri, mfalme wa Soba,
10 akampeleka mwanawe Hadoramu kwa mfalme Daudi, ili kumsalimia, na kumbarikia, kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou; naye akaleta vyombo vya dhahabu, na fedha, na shaba, vya namna zote.
11 Hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha na dhahabu, aliyoteka nyara kwa mataifa yote; kwa Edomu, na kwa Moabu, na kwa wana wa Amoni, na kwa Wafilisti, na kwa Amaleki.
12 Tena Abishai, mwana wa Seruya, akawapiga wa Waedomi katika Bonde la Chumvi watu kumi na nane elfu.
13 Akaweka ngome katika Edomu; na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda, kila alikokwenda.
14 Basi Daudi akatawala juu ya Israeli wote; akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.
15 Na Yoabu mwana wa Seruya akawa juu ya jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe.
16 Na Sadoki mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki mwana wa Abiathari, walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;
17 na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; na wana wa Daudi walikuwa wakuu kumzunguka mfalme.

1 Nyakati 19


1 Ikawa baada ya hayo, Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, akafa, akamiliki mwanawe mahali pake.
2 Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahashi, kwa kuwa babaye alinitendea mimi wema. Basi Daudi akapeleka wajumbe ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni kwa Hanuni, ili wamtulize.
3 Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, Je! Waona Daudi amheshimu babayo kwa kukupelekea wafariji? Je! Hawakukujia watumishi wake ili kuiangalia nchi, na kuiangamiza, na kuipeleleza?
4 Basi Hanuni akawatwaa watumishi wa Daudi, akawanyoa, akawakatia nguo zao katikati, hata matakoni, akawatoa waende zao.
5 Wakaenda watu wakamwambia Daudi jinsi walivyotendewa wale watu. Naye akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi.
6 Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakapeleka talanta elfu za fedha ili kujiajiria magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba.
7 Basi wakajiajiria magari thelathini na mbili elfu, na mfalme wa Maaka na watu wake; nao walikuja wakatua mbele ya Medeba. Na wana wa Amoni wakakusanyika kutoka miji yao, wakaja vitani.
8 Basi Daudi aliposikia habari akamtuma Yoabu, na jeshi lote la mashujaa.
9 Wakatoka wana wa Amoni, wakapanga vita langoni pa mji; na hao wafalme waliokuja walikuwa peke yao uwandani.
10 Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami.
11 Na hao watu waliosalia akawatia mikononi mwa Abishai, nduguye, nao wakajipanga juu ya wana wa Amoni.
12 Akasema, Wakiwa Washami ni hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia; lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakusaidia wewe.
13 Uwe hodari, tukajitie moyo mkuu kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye Bwana afanye yaliyo mema machoni pake.
14 Basi Yoabu, na watu waliokuwa pamoja naye, wakakaribia kupigana na Washami; nao wakakimbia mbele yake.
15 Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, nduguye, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akaja Yerusalemu.
16 Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakapeleka wajumbe, wakawavuta Washami walioko ng'ambo ya Mto, na Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza.
17 Alipoambiwa Daudi; akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye.
18 Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari saba elfu, na askari waendao kwa miguu arobaini elfu, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.
19 Na watumwa wa Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Daudi, wakamtumikia; wala Washami hawakukubali kuwasaidia wana wa Amoni tena.

1 Nyakati 20


1 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza.
2 Kisha Daudi akamtwalia mfalme wao taji toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.
3 Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawakata-kata kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.
4 Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gobu; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai; nao wakashindwa.
5 Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti ,ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.
6 Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.
7 Naye huyo alipowatukana Israeli, Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua.
8 Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi,nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi , na kwa mkono wa watumishi wake.

1 Nyakati 21


1 Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.
2 Basi Daudi akamwambia Yoabu, na wakuu wa watu, Nendeni kawahesabu Israeli toka Beer-sheba mpaka Dani; mkanipashe habari, nipate kujua jumla yao.
3 Naye Yoabu akasema, Bwana na awaongeze watu wake mara mia hesabu yao ilivyo; lakini, bwana wangu mfalme, si wote watumishi wa bwana wangu? Mbona basi bwana wangu analitaka neno hili? Mbona awe sababu ya hatia kwa Israeli?
4 Lakini neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu. Kwa hiyo Yoabu akaenda zake, akapita kati ya Israeli wote, akafika Yerusalemu.
5 Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu mia nne na sabini elfu, wenye kufuta panga.
6 Lakini Lawi na Benyamini hakuwahesabu miongoni mwao; kwa sababu neno la mfalme limemchukiza Yoabu.
7 Neno hilo likawa baya machoni pa Mungu; kwa hiyo akawapiga Israeli.
8 Naye Daudi akamwambia Mungu, Nimekosa sana, kwa kuwa nimelifanya jambo hili; lakini sasa uuondolee mbali, nakusihi, uovu wa mtumwa wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.
9 Naye Bwana akanena na Gadi, mwonaji wake Daudi, akisema,
10 Nenda ukanene na Daudi, ukisema, Bwana asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya ujichagulie moja, nikutendee hilo.
11 Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo;
12 miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.
13 Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.
14 Basi Bwana akawaletea Israeli tauni; nao wakaanguka wa Israeli watu sabini elfu.
15 Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, Bwana akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa Bwana akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
16 Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa Bwana amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusakmu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifulifuli, nao wamevaa nguo za magunia.
17 Daudi akamwambia Mungu, Je! Si mimi niliyeamuru watu wahesabiwe? Naam, mimi ndimi niliyekosa, na kufanya yaliyo maovu sana; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako, nakusihi, Ee Bwana, Mungu wangu, na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya babangu; wala si juu ya watu wako, hata wao wapigwe.
18 Ndipo huyo malaika wa Bwana akamwamuru Gadi kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie Bwana madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
19 Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, alilolinena kwa jina la Bwana.
20 Arauna alipogeuka, na kumwona yule malaika, ndipo yeye na wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha. Naye Arauna alikuwa akipura ngano.
21 Basi Daudi alipokuwa akimjia Arauna, Arauna akatazama, akamwona Daudi, akatoka katika kile kiwanja, akamsujudia Daudi kifulifuli hata nchi.
22 Ndipo Daudi akamwambia Arauna, Unipe mahali pa kiwanja hiki, ili kwamba nimjengee Bwana madhabahu hapa; kwa thamani yake kamili utanipa; ili kwamba tauni izuiliwe katika watu.
23 Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng'ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa.
24 Mfalme Daudi akamwambia Arauna, La, sivyo, lakini kweli nitazinunua kwa thamani yake kamili; kwani sitamtwalia Bwana kilicho chako, wala kutoa sadaka ya kuteketezwa isiyo na gharama.
25 Basi Daudi akampimia Arauna thamani ya mahali pale shekeli mia sita za dhahabu kwa uzani
26 Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana Bwana; naye akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu hiyo ya sadaka ya kuteketezwa.
27 Bwana naye akamwamuru malaika; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena.
28 Wakati huo, Daudi alipoona ya kwamba Bwana amemwitikia katika kiwanja cha Arauna, Myebusi, ndipo hutoa dhabihu huko.
29 Kwa maana ile maskani ya Bwana, aliyoifanya Musa jangwani, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, vilikuwapo wakati huo mahali pa juu pa Gibeoni.
30 Wala Daudi hakuweza kwenda mbele yake ili kumwuliza Mungu; kwa sababu aliona hofu kwa ajili ya upanga wa yule malaika wa Bwana.

1 Nyakati 22


1 Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya Bwana Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa Israeli.
2 Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu.
3 Daudi akaweka akiba tele ya chuma kwa misumari ya tarabe za malango, na kwa mafungo; na ya shaba akiba tele isiyo na uzani;
4 na mierezi isiyo na idadi; kwa kuwa Wasidoni na watu wa Tiro wakamletea Daudi mierezi tele.
5 Daudi akasema, Sulemani mwanangu akali ni mchanga bado, na mwororo, nayo nyumba atakayojengewa Bwana haina budi kuwa nzuri mno, yenye sifa na yenye fahari katika nchi zote; kwa hiyo mimi nitaiwekea akiba. Basi Daudi akaweka akiba tele kabla hajafa.
6 Ndipo akamwita Sulemani mwanawe, akamwagiza amjengee Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba.
7 Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wangu.
8 Lakini neno la Bwana likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;
9 tazama, utazaliwa mwana, atakayekuwa mtu wa kustarehe; nami nitamstarehesha mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake ;
10 huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakifanya imara milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.
11 Sasa mwanangu, Bwana na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya Bwana, Mungu wako, kama alivyonena kwa habari zako.
12 Bwana na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike torati ya Bwana, Mungu wako.
13 Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, Bwana alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.
14 Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya Bwana, talanta elfu mia za dhahabu, na talanta elfu elfu za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.
15 Tena kwako kuna mafundi wengi, wenye kuchonga na kufanyiza kazi ya mawe na miti, na kila aliye mstadi kwa kazi yo yote;
16 ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye Bwana na awe pamoja nawe.
17 Tena Daudi akawaamuru wakuu wote wa Israeli, kwamba wamsaidie Sulemani mwanawe, akisema,
18 Je! Si Bwana, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwastarehesha pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za Bwana, na mbele ya watu wake.
19 Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta Bwana, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee Bwana Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la agano la Bwana, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la Bwana.

1 Nyakati 23


1 Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli.
2 Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.
3 Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.
4 Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya Bwana; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;
5 na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu Bwana kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.
6 Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.
7 Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.
8 Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu.
9 Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya mbari za baba za Ladani.
10 Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei.
11 Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja.
12 Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.
13 Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za Bwana, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
14 Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.
15 Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri.
16 Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.
17 Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
18 Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.
19 Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
20 Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.
21 Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.
22 Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23 Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.
24 Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya Bwana, wenye miaka ishirini na zaidi.
25 Kwa kuwa Daudi alisema, Bwana, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;
26 wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.
27 Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi.
28 Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya Bwana, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu;
29 tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;
30 nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana, na jioni vivyo hivyo;
31 na kumtolea Bwana sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za Bwana;
32 tena walinde ulinzi wa hema ya kukutania, na ulinzi wa patakatifu, na ulinzi wa wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya Bwana.

1 Nyakati 24


1 Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.
2 Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani.
3 Akawagawanya Daudi, na Sadoki wa wana wa Eleazari, na Ahimeleki wa wana wa Ithamari, katika utumishi kwa kadiri ya usimamizi wao.
4 Wakaonekana wakuu wengi wa wana wa Eleazari kuliko wa wana wa Ithamari; wakagawanyika hivi; wa wana wa Eleazari kulikuwa na kumi na sita, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao; na wa wana wa Ithamari, sawasawa na mbari za baba zao, wanane.
5 Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.
6 Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.
7 Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya;
8 ya tatu Harimu, ya nne Seorimu;
9 ya tano Malkia, ya sita Miyamini;
10 ya saba Hakosi, ya nane Abia;
11 ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania;
12 ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu;
13 ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu;
14 ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri;
15 ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi;
16 ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli;
17 ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli;
18 ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.
19 Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa Bwana kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.
20 Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya.
21 Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao.
22 Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.
23 Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne.
24 Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri.
25 Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria.
26 Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno.
27 Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri.
28 Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana.
29 Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli.
30 Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata mbari za baba zao.
31 Hao nao wakatupiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa mbari za baba za makuhani na za Walawi; mbari za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.

1 Nyakati 25


1 Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi sawasawa na utumishi wao;
2 wa wana wa Asafu; Zakuri, na Yusufu, na Nethania, na Asharela, wana wa Asafu; walioamriwa na Asafu, aliyetabiri kwa amri ya mfalme.
3 Wa Yeduthuni; wana wa Yeduthuni; Gedalia, na Seri, na Yeshaya, na Hashabia, na Matithia, [na Shimei], watu sita; walioamriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi, aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu Bwana.
4 Wa Hemani; wana wa Hemani; Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, na Romanti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri, Mahaziothi;
5 hao wote ndio wana wa Hemani, mwonaji wa mfalme, kwa maneno ya Mungu, ili kuinua pembe. Naye Mungu akampa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.
6 Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa Bwana, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.
7 Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia Bwana, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.
8 Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.
9 Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili;
10 ya tatu Zakuri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
11 ya nne Seri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
12 ya tano Nethania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
13 ya sita Bukia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
14 ya saba Asharela, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
15 ya nane Yeshaya, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
16 ya kenda Matania wanawe na nduguze, kumi na wawili;
17 ya kumi Shimei, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
18 ya kumi na moja Uzieli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
19 ya kumi na mbili Hashabia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
20 ya kumi na tatu Shebueli, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
21 ya kumi na nne Matithia, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
22 ya kumi na tano Yeremothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
23 ya kumi na sita Hanania, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
24 ya kumi na saba Yoshbekasha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
25 ya kumi na nane Hanani, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
26 ya kumi na kenda Malothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
27 ya ishirini Eliatha, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
28 ya ishirini na moja Hothiri, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
29 ya ishirini na mbili Gidalti, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
30 ya ishirini na tatu Mahaziothi, wanawe na nduguze, kumi na wawili;
31 ya ishirini na nne Romanti-ezeri, wanawe na nduguze, kumi na wawili.

1 Nyakati 26


1 Kwa zamu zao mabawabu; wa Wakora; Meshelemia mwana wa Kore, wa wana wa Ebiasafu.
2 Naye Meshelemia alikuwa na wana; Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wa pili, Zebadia wa tatu, Yathnieli wa nne;
3 Elamu wa tano, Yohana wa sita, Elioenai wa saba.
4 Naye Obed-edomu alikuwa na wana; Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili, Yoa wa tatu, na Sakari wa nne, na Nethaneli wa tano;
5 Amieli wa sita, Isakari wa saba, Peulethai wa nane; kwa jinsi Mungu alivyombariki.
6 Naye mwanawe Shemaya akazaliwa wana, waliomiliki juu ya mbari ya baba yao; kwa kuwa walikuwa waume mashujaa.
7 Wana wa Shemaya; Othni, na Refaeli, na Obedi, na Elzabadi, nduguze walikuwa mashujaa, Elihu, na Semakia.
8 Hao wote walikuwa wana wa Obed-edomu; wao na wana wao na ndugu zao, watu hodari wawezao huo utumishi; watu wa Obed-edomu sitini na wawili.
9 Naye Meshelemia alikuwa na wana na nduguze, watu mashujaa, kumi na wanane.
10 Hosa naye, wa wana wa Merari, alikuwa na wana; Shimri mkuu wao; (kwani ajapokuwa yeye si mzaliwa wa kwanza, babaye alimweka mkuu);
11 Hilkia wa pili, Tebalia wa tatu, Zekaria wa nne; wana wote wa Hosa pamoja na nduguze walikuwa watu kumi na watatu.
12 Katika hao zilikuwa zamu za mabawabu, yaani, katika hao wakuu, wenye ulinzi sawasawa na ndugu zao, wa kutumika katika nyumba ya Bwana.
13 Nao wakatupiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo sawasawa na wakubwa, kwa kadiri ya mbari za baba zao.
14 Kura ya mashariki ya lango ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini.
15 Ya Obed-edomu ya kusini; na ya wanawe nyumba ya akiba.
16 Ya Shupimu na Hosa upande wa magharibi, langoni pa Shalekethi, hapo penye daraja ya kupandia, ulinzi kwa ulinzi.
17 Upande wa mashariki walikuwapo Walawi sita, kaskazini wanne kila siku, kusini wanne kila siku, na wa nyumba ya akiba wawili wawili.
18 Penye Parbari upande wa magharibi, walikuwapo wanne darajani, na wawili huko Parbari.
19 Hizo ndizo zamu za mabawabu; wa wana wa Wakora, na wa wana wa Merari.
20 Na katika Walawi; Ahia alikuwa juu ya hazina za nyumba ya Mungu, na juu ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.
21 Wana wa Ladani; wana wa Wagershoni waliokuwa wa Ladani; wakuu wa mbari za mababa waliokuwa wa Ladani, Mgershoni; Yehieli.
22 Wana wa Yehieli; Zethamu, na Yoeli nduguye, juu ya hazina za nyumba ya Bwana.
23 Wa Waamramu, wa Waishari, wa Wahebroni, wa Wauzieli;
24 na Shebueli, mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, alikuwa mtawala hazina zote.
25 Na nduguze; wa Eliezeri, Rehabia mwanawe, na Ishia mwanawe, na Yoramu mwanawe, na Zikri mwanawe, na Shelomothi mwanawe.
26 Huyo Shelomothi na ndugu zake walikuwa juu ya hazina zote za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyoviweka wakfu mfalme Daudi, na hao wakuu wa mbari za mababa, na maakida wa maelfu na wa mamia, na maakida wa jeshi.
27 Katika nyara zilizopatikana vitani, waliweka wakfu sehemu, ili kuitengeneza nyumba ya Bwana.
28 Na vyote alivyoviweka wakfu Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, na Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya; na mtu ye yote aliyekiweka wakfu kitu cho chote, kilikuwa chini ya mkono wa Shelomothi na nduguze.
29 Katika Waishari, Kenania na wanawe walikuwa kwa ajili ya kazi ya nje juu ya Israeli, kuwa maakida na makadhi.
30 Katika Wahebroni, Hashabia na nduguze, mashujaa, elfu na mia saba, walikuwa na usimamizi juu ya Israeli ng'ambo ya Yordani upande wa magharibi; kwa ajili ya kazi zote za Bwana, na kwa utumishi wa mfalme.
31 Katika Wahebroni Yeria alikuwa mkuu, yaani, wa hao Wahebroni kwa kufuata vizazi vyao kwa mbari za mababa. Katika mwaka arobaini wa kutawala kwake Daudi wakatafutwa, wakaonekana huko Yazeri ya Gileadi miongoni mwao waume mashujaa.
32 Na nduguze, mashujaa, walikuwa elfu mbili na mia saba, wakuu wa mbari za mababa, ambao mfalme Daudi aliwaweka wawe wasimamizi juu ya Wareubeni, na Wagadi, na nusu kabila ya Wamanase, kwa ajili ya kila neno lililomhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.

1 Nyakati 27


1 Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa mbari za mababa, na maakida wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lo lote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu ishirini na nne elfu.
2 Juu ya zamu ya kwanza ya mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu, mwana wa Zabdieli; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
3 Yeye alikuwa wa wana wa Peresi, mkuu wa maakida wote wa jeshi mwezi wa kwanza.
4 Na juu ya zamu ya mwezi wa pili alikuwa Dodai, Mwahohi, na zamu yake; na Miklothi alikuwa amiri; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
5 Akida wa tatu wa jeshi mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa Yehoyada, kuhani; alikuwa mkuu, na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
6 Huyo Benaya ndiye yule aliyekuwa shujaa wa wale thelathini, na juu ya wale thelathini; na katika zamu yake alikuwa Amizabadi mwanawe.
7 Akida wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, nduguye Yoabu, na Zebadia mwanawe baada yake; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
8 Akida wa tano wa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi, Mwizrahi; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
9 Akida wa sita wa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
10 Akida wa saba wa mwezi wa saba alikuwa Heksi, Mpeloni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
11 Akida wa nane wa mwezi wa nane alikuwa Sibekai, Mhushathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
12 Akida wa kenda wa mwezi wa kenda alikuwa Abiezeri, Mwanathothi, wa Wabenyamini; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
13 Akida wa kumi wa mwezi wa kumi alikuwa Maharai, Mnetofathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
14 Akida wa kumi na moja wa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya, Mpirathoni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
15 Akida wa kumi na mbili wa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heledi, Mnetofathi, wa Othnieli; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
16 Tena wakuu wa kabila za Israeli walikuwa hawa; wa Wareubeni, Eliezeri mwana wa Zikri; wa Wasimeoni, Shefatia mwana wa Maaka;
17 wa Lawi, Hashabia mwana wa Kemueli; wa Haruni, Sadoki;
18 wa Yuda, Elihu, mmojawapo wa nduguze Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli;
19 wa Zabuloni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeromothi mwana wa Azrieli;
20 wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia, wa nusu kabila ya Manase, Yoeli mwana wa Pedaya;
21 wa nusu kabila ya Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri;
22 wa Dani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao walikuwa maakida wa kabila za Israeli.
23 Lakini Daudi hakufanya hesabu yao wenye miaka ishirini na waliopungua; kwa kuwa Bwana alikuwa amesema, ya kwamba atawaongeza Israeli mfano wa nyota za mbinguni.
24 Yoabu, mwana wa Seruya, akaanza kuhesabu, lakini hakumaliza; na ghadhabu ikawapata Israeli kwa hayo; wala haikuhesabiwa hesabu hiyo ndani ya taarifa za mfalme Daudi.
25 Na juu ya hazina za mfalme alikuwa Azmawethi mwana wa Adieli; na juu ya hazina za mashambani, za mijini, na vijijini, na ngomeni, alikuwa Yonathani mwana wa Uzia;
26 na juu ya hao wenye kazi ya shamba kuilima ardhi alikuwa Ezri mwana wa Kelubu;
27 na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi;
28 na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi;
29 na juu ya makundi ya ng'ombe waliolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya makundi waliokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai;
30 na juu ya ngamia alikuwa Obili, Mwishmaeli; na juu ya punda alikuwa Yedeya, Mmeronothi;
31 na juu ya makundi ya kondoo alikuwa Yazizi, Mhagri. Hao wote walikuwa maakida wa akiba alizokuwa nazo mfalme Daudi.
32 Naye Yonathani, mjombawe Daudi, alikuwa mshauri, na mtu wa akili, na mwandishi; Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa pamoja na wana wa mfalme;
33 na Ahithofeli alikuwa mshauri wake mfalme; na Hushai, Mwarki, alikuwa rafiki yake mfalme;
34 na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu.

1 Nyakati 28


1 Kisha Daudi akawakusanya huko Yerusalemu wakuu wote wa Israeli, wakuu wa kabila, na maakida wa vikosi wenye kumtumikia mfalme kwa zamu, na maakida wa maelfu, na maakida wa mamia, na wenye kutawala juu ya mali na milki za mfalme, na za wanawe, pamoja na matowashi, na mashujaa, naam, waume mashujaa wote.
2 Ndipo Daudi mfalme akasimama kwa miguu yake, akasema, Nisikilizeni, ndugu zangu, na watu wangu; Mimi nalikuwa na nia ya kuijenga nyumba ya kustarehe kwa ajili ya sanduku la agano la Bwana, na kiti cha kuwekea miguu yake cha Mungu wetu; hata nalikuwa nimeweka tayari kwa kujenga.
3 Lakini Mungu akaniambia, Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umekuwa mtu wa vita, nawe umemwaga damu.
4 Walakini Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote;
5 tena katika wana wangu wote (kwani Bwana amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa Bwana, juu ya Israeli.
6 Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye.
7 Na ufalme wake nitauweka imara milele, akijitia kwa bidii kuzitenda amri zangu na hukumu zangu, kama hivi leo.
8 Basi sasa, machoni pa Israeli wote, hilo kusanyiko la Bwana, na masikioni pa Mungu wetu, angalieni na kuzitafuta amri zote za Bwana, Mungu wenu, ili mpate kuimiliki nchi hii njema, na kuwarithisha wana wenu baada yenu hata milele.
9 Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.
10 Jihadhari basi; kwani Bwana amekuchagua wewe ili ujenge nyumba itakayokuwa mahali patakatifu; uwe hodari ukatende hivyo.
11 Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na orofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema;
12 na mfano wa yote aliyokuwa nayo kwa roho, katika habari ya nyua za nyumba ya Bwana, na ya vyumba vyote vilivyoizunguka, ya hazina za nyumba ya Mungu, na ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu;
13 tena katika habari ya zamu za makuhani na Walawi, na ya kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya Bwana, na ya vyombo vyote vya utumishi nyumbani mwa Bwana;
14 ya dhahabu kwa uzani kwa vyombo vya dhahabu, kwa vyombo vyote vya utumishi wa kila namna; ya fedha kwa uzani kwa vyombo vyote vya fedha, kwa vyombo vyote vya utumishi wa kila namna;
15 kwa uzani tena kwa vinara vya dhahabu, na kwa taa zake za dhahabu, kwa uzani, kwa kila kinara, na kwa taa zake; na kwa vinara vya fedha, kwa uzani kwa kila kinara na kwa taa zake, kwa kadiri ya matumizi ya kila kinara;
16 na dhahabu kwa uzani kwa meza za mikate ya wonyesho, kwa kila meza; na fedha kwa meza za fedha;
17 na nyuma, na mabakuli, na vikombe vya dhahabu safi; na kwa matasa ya dhahabu, kwa uzani kwa kila tasa; na kwa matasa ya fedha, kwa uzani kwa kila tasa;
18 na kwa madhabahu ya kufukizia, dhahabu iliyosafika sana kwa uzani; na dhahabu kwa mfano wa gari, yaani, makerubi, yenye kutandaza mabawa, na kulifunika sanduku la agano la Bwana.
19 Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa Bwana, naam, kazi zote za mfano huu.
20 Kisha Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; yeye hatakupungukia wala kukuacha, hata itakapomalizika kazi yote ya huo utumishi wa nyumba ya Bwana.
21 Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wo wote; tena maakida na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.

1 Nyakati 29


1 Kisha mfalme Daudi akawaambia kusanyiko lote, Sulemani mwanangu, ambaye Mungu amemchagua peke yake, akali ni mchanga bado na mwororo, nayo kazi hii ni kubwa; kwani nyumba hii ya enzi si kwa mwanadamu, ila kwa Bwana, Mungu.
2 Basi kwa uwezo wangu wote nimeiwekea akiba nyumba ya Mungu wangu, dhahabu kwa vitu vya dhahabu, na fedha kwa vitu vya fedha, na shaba kwa vitu vya shaba, na chuma kwa vitu vya chuma, na miti kwa vitu vya miti; vito vya shohamu, na vya kujazia, vito vya njumu, na vya rangi mbalimbali, na mawe ya thamani ya kila namna, na marimari tele.
3 Nami tena kwa kuwa nimeiwekea nyumba ya Mungu wangu shauku yangu, nami ninayo hazina yangu mwenyewe ya dhahabu na fedha, naitoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, zaidi ya hiyo akiba niliyoiwekea tayari nyumba takatifu;
4 yaani, talanta elfu tatu za dhahabu, za dhahabu ya Ofiri, na talanta elfu saba za fedha iliyosafika, ya kuzifunikiza kuta za nyumba;
5 ya dhahabu, kwa vitu vya dhahabu, na ya fedha kwa vitu vya fedha, na kwa kazi za kila namna zitakazofanywa kwa mikono ya mafundi. Ni nani basi ajitoaye kwa moyo ili ajiweke wakfu leo kwa Bwana?
6 Ndipo wakuu wa mbari za mababa, na wakuu wa kabila za Israeli, na maakida wa maelfu na wa mamia, pamoja na wasimamizi wa kazi ya mfalme, wakajitoa kwa hiari yao;
7 nao wakatoa, kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu, dhahabu talanta elfu tano, na darkoni elfu kumi,na fedha taranta elfu kumi, na shaba taranta elfu kumi na nane ,na chuma taranta elfu mia.
8 Na wale walioonekana kuwa na vito vya thamani wakavitoa vitiwe katika hazina ya nyumba ya Bwana, chini ya mkono wa Yehieli, Mgershoni.
9 Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu.
10 Kwa hiyo Daudi akamhimidi Bwana, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele.
11 Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
12 Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.
13 Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu.
14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.
15 Kwani sisi tu wageni mbele zako, na wasafiri, kama walivyokuwa baba zetu wote; ni kama kivuli siku zetu duniani, wala taraji ya kukaa hapana.
16 Ee Bwana, Mungu wetu, akiba hii yote tuliyoiweka, ili tukujengee nyumba kwa ajili ya jina lako takatifu, yatoka yote mkononi mwako, na yote ni yako wewe.
17 Nami najua, Mungu wangu, ya kuwa wewe wajaribu moyo, nawe wapendezwa na unyofu. Nami katika unyofu wa moyo wangu nimeyatoa haya yote kwa hiari yangu mwenyewe; nami sasa nimeona kwa furaha watu wako, waliopo hapa, wakikutolea kwa hiari yao.
18 Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, baba zetu, ulilinde jambo hili milele katika fikira za mawazo ya mioyo ya watu wako, ukaiongoze mioyo yao kwako;
19 naye Sulemani mwanangu, umpe moyo mkamilifu, ili azishike amri zako, na shuhuda zako, na maagizo yako, akayatende hayo yote na kuijenga nyumba hii ya enzi, niliyoiwekea akiba.
20 Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, Haya, mhimidini Bwana, Mungu wenu. Basi kusanyiko lote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao, wakainama vichwa vyao, wakamsujudia Bwana, na mfalme naye.
21 Wakamtolea Bwana dhabihu, wakamchinjia Bwana sadaka za kuteketezwa, siku ya pili yake, yaani, ng'ombe elfu, na kondoo waume elfu, na wana-kondoo elfu, pamoja na sadaka zao za vinywaji, na dhabihu nyingi kwa ajili ya Israeli wote;
22 wakala na kunywa mbele za Bwana siku ile, kwa furaha kuu. Wakamtawaza Sulemani, mwana wa Daudi, mara ya pili, wakamtia mafuta mbele za Bwana, awe mkuu, na Sadoki awe kuhani.
23 Ndipo Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Bwana, awe mfalme badala ya Daudi babaye, akafanikiwa; nao Israeli wote wakamtii.
24 Nao wakuu wote, na mashujaa, na wana wote wa mfalme Daudi nao, wakajitia chini ya mfalme Sulemani.
25 Naye Bwana akamtukuza Sulemani mno machoni pa Israeli wote, akampa fahari ya kifalme ya kumpita mfalme awaye yote aliyekuwa kabla yake katika Israeli.
26 Basi Daudi, mwana wa Yese, akawa mfalme juu ya Israeli wote.
27 Na wakati aliotawala juu ya Israeli, ulikuwa miaka arobaini; miaka saba alitawala Hebroni, na miaka thelathini na mitatu akatawala Yerusalemu.
28 Akafa mwenye umri mwema, ameshiba siku, na mali, na heshima; naye Sulemani mwanawe akamiliki badala yake.
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika tarehe ya Samweli, mwonaji, na katika tarehe ya Nathani, nabii, na katika tarehe ya Gadi, mwonaji;
30 pamoja na kutawala kwake kote na nguvu zake, nazo zamani zilizompata yeye, na Israeli, na falme zote za nchi.